Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania – TAWIRI, Dkt.David Manyanza ameishukuru Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kutoa magari mapya matatu kwa ajili ya shughuli za tafiti za wanyamapori.
Dkt.Manyanza ameeleza TAWIRI imeendelea kuhakikisha tafiti za wanyamapori zinafanyika kwa ufanisi mkubwa ili kuimarisha uhifadhi na kukuza utalii ambapo kupitia mapato yake ya ndani imenunua magari mapya mawili na kufanya jumla ya magari mapya kuwa matano (5).
Aidha, Dkt. Manyanza ameipongeza Menejimenti kwa mchango wao na kutoa wito magari hayo kutumika kwa ufanisi ili kuleta tija kwa Taasisi .
Naye Mkurugenzi Mkuu wa TAWIRI Dkt. Eblate Mjingo ameishukuru Serikali kwa kutoa magari hayo ambayo yatapungunguza changamoto ya vitendea kazi katika utekelezaji wa shughuli za utafiti.
Aidha, Dkt.Mjingo amesema katika magari hayo matano magari mawili yamenunuliwa kwa mapato ya ndani.
Magari hayo matano ni aina ya Land Cruiser LX mbili (2) , Land Cruiser Double Cabin moja (1) na Land Cruiser Hard Top mbili (2).