MUHIMU KUFAHAMU CHIMBUKO LA BOMU BARIDI LA KUONDOA TEMBO KWENYE MAENEO YA WATU NI UBORESHAJI WA MBINU ZILIZOKUWA ZIKITUMIKA AWALI

Bomu Baridi la kuondoa tembo kwenye maeneo ya watu ni maboresho ya mbinu/dhana zilizokuwa zikitumika awali ambapo kwa mujibu wa utafiti zilionekana kuwa na ufanisi mdogo kwa baadhi ya maeneo kutokana na wanyamapori hususan tembo kuwa na uwezo mkubwa wa akili na hivyo kuzoea mbinu hizo. Kufuatia hali hiyo, ikaonekana kuna haja ya kuboresha mbinu/dhana hizo kwa kuimarisha kifungashio, kishindo na namna ya ulipukaji ndipo ubunifu wa bomu baridi ukafanyika.

Muhimu, mabomu baridi yanatumika kuondoa tembo kwenye maeneo ya watu na si ndani ya hifadhi

Kama lilivyo jina lake bomu baridi, bomu hili ni salama kwani linatumika nje ya hifadhi na kwa tembo lina usumbufu wa harufu ya pilipili, sauti, na miale ya mwanga inayotoka nyakati za usiku. Pia, bomu hili ni tofauti na mabomu tuliyoyazoea ambayo mlipuko wake ni moto, kishindo kikubwa, na kujeruhi.

Ikumbukwe miongoni mwa mbinu/dhana zilizoibuliwa awali za kuwazuia na kuwaondoa tembo kwenye maeneo ya watu ni pamoja na matumizi ya vifaa vyenye sauti (Vuvuzela), vilipuzi vyenye mchanganyo wa pilipili (bomu la pilipili), vifaa vyenye mlipuko na sauti (mafataki), tochi zenye mwanga mkali na mwanga wa rangi tofauti, fensi ya vitambaa vya oili chafu na pilipili, matofali ya pilipili, teknolojia ya helikopta nk.

Aidha, bomu baridi ni maboresho ya dhana tajwa hapo juu na utafiti unaendelea ili kuimarisha dhana hii mpya na maoni ya wadau yanapokelewa kwa uboreshaji

Visitors

031676
Users Today : 7
Users Last 7 days : 399
Users This Month : 1192
Total Users : 31676

Office Location

Contact Us