KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI, TAWIRI  YABAINISHA MCHANGO WA WADUDU KWENYE  MAZINGIRA

Ikiwa leo tarehe  05.06.2024 ni maadhimisho ya Siku ya  Mazingira Duniani ambapo Kitaifa yamefanyika Jijini  Dodoma, Taasisi ya Utafiti wa  Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) imebainisha mchango mkubwa wa wadudu mbalimbali akiwemo  nyuki katika Mazingira.

Akitoa elimu ya wadudu kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi NALOPA waliotembelea Makao Makuu ya TAWIRI Mtafiti Alphoncinah Mponzi amesema, wadudu wana mchamgo mkubwa katika mazingira ambapo wanasaidia uchavushaji  wa mimea  kwa zaidi ya asilimia  80%.

“Nyuki ni mchavushaji mkuu wa kuendeleza uwepo wa mimea mbalimbali katika uhifadhi” ameeleza Mtafiti Mponzi

Aidha, Mtafiti Mponzi amesema mbali na uchavushaji wadudu wanasaidia uozeshaji wa taka na usafishaji wa mazingira pamoja na uoteshaji wa mbegu mbalimbali ambapo amebainisha mdudu (_Dung beetle_) anasaidia utawanyaji na uoteshaji mbegu mwituni, umeng’enyaji virutubisho vya udongo hasa vinyesi vya wanyama,(_decomposition_) na uongezaji mbolea kwenye udongo (soil fertilization) hivyo  kufanya hivi husaidia kuwezesha makazi ya wanyama wengine.

Vilevile, alieleza kuwa uwepo wa wadudu katika uhifadhi kunasaida mzunguko wa chakula (_food chain_) ambapo kuna wanyama wadogo na ndege wanaotegemea wadudu kwa asilimia kubwa kama chakula chao akiwemo mnyama mhanga (_Aardvark_) na  wanyama hawa  huliwa na wanyama wengine.

Naye, Mwalimu Charles Mollel kutoka shule ya  Msingi NALOPA ameishukuru TAWIRI kuanza kutoa elimu ya wadudu na nyuki kwa wanafunzi wa Darasa la Saba wa shule hiyo ambayo  ina Mkakati wa  kuhakikisha wanafunzi wanajifunza kwa vitendo zaidi.

*Muhimu*,✍️ mazingira ni pamoja na mimea ambapo kwa mujibu wa  tafiti uchavushaji wa  mimea mbalimbali  unafanywa na wadudu  kwa asilimia 80%.

Visitors

031678
Users Today : 9
Users Last 7 days : 401
Users This Month : 1194
Total Users : 31678

Office Location

Contact Us