KUELEKEA SIKU YA WANYAMAPORI DUNIANI WADAU WAJADILI MATUMIZI YA TEKNOLOJIA KATIKA UHIFADHI

Watafiti na Wahifadhi nchini wanakutana kwa siku mbili jijini Arusha kwa lengo la kujadili na kuja na mikakati ya pamoja ya kuimarisha uhifadhi na kukuza utalii nchini kuelekea Siku ya Wanyamapori Duniani ambayo huadhimishwa Machi 03 kila mwaka.

Akifungua mkutano huo ambao umeratibiwa na Wizara ya Maliasili na Utalii, Kaimu Mkurugenzi Idara ya Wanyamapori Dkt. Fortunata Msoffe amefafanua kuwa wakati Taifa likiwa kwenye maombelezo ya kifo cha aliyekuwa Rais wa awamu ya pili hayati Ali Hassan Mwinyi ni muhimu kwa wahifadhi na watanzania kwa ujumla kuenzi jitihada za viongozi katika kutunza Maliasili ya Wanyamapori kwa taifa letu.

Aidha, amesisitiza kuwa viongozi wakuu wa Tanzania ikiwa ni pamoja na hayati Mzee Mwinyi wamekuwa na mchango mkubwa kwenye uhifadhi wa raslimali za wanyapoli kuanzia awamu ya kwanza ya baba wa Taifa hadi sasa ambapo Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa mhifadhi namba moja mwenye maono makubwa kwenye Uhifadhi wa raslimali na kukuza Utalii nchini.

“Hapa naomba nisisitize kuwa wamefanya jitihada kubwa kuhakikisha Maliasili inakuwepo kwa kizazi kilichopita ,kilichopo na kijacho ili ziendelee kunufaisha Taifaletu” Amefafanua Dkt. Msofe .

Mkutano huo umejumuisha Watafiti na Wahifadhi kutoka Idara za Wanyamapori, Misitu na Malikale, Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI),Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), Mamlaka ya Uhifadhi Ngorongoro (NNCAA), Mamlaka ya Uhifadhi wa Wanyamapori (TAWA), Wakala wa huduma za Misitu (TFS), Chuo cha Wanyamapori Mweka na wadau kutoka taasisi zisizo za kiserikali za WWF, FZS, CWMAC, Nature Tanzania, TNRF na AWF.

Kaulimbiu ni ya siku ya wanyamapori duniani kwa mwaka huu ni ‘ “UNGANISHA WATU NA ULIMWENGU: VUMBUA MATUMIZI YA TEKNOLOJIA YA KIDIGITALI KATIKA UHIFADHI WA WANYAMAPORI”

Visitors

031670
Users Today : 1
Users Last 7 days : 393
Users This Month : 1186
Total Users : 31670

Office Location

Contact Us