Tanzania inaendeleaa kujivunia kuwa na utajiri mkubwa wa Maliasili ya Wanyamapori ambapo jitihada kubwa zinaendelea kufanyika kulinda rasilimali hii kwa kizazi kilichopo na kijacho .
Miongoni mwa jitihada hizo ni pamoja na kufanya sensa ya wanyamapori ambayo ni muhimu katika kubaini uwepo na idadi ya wanyamapori, mtawanyiko pamoja na viashiria hatarishi katika afya ya mfumo ikolojia sambamba na kutathmini ufanisi wa mikakati ya uhifadhi.
Aidha, kupitia Matokeo sensa za wanyamapori katika mifumo mitatu (3) ya ikolojia ya Nyerere-Selous-Mikumi, Saadani-Wamimbiki na Serengeti yaliyotangwaza siku ya jana 22.04.2024 na Mhe.Angellah Kairuki, Waziri wa Maliasili na Utalii yanadhihirisha kuendelea kuimarisha kwa uhifadhi nchini na jitihada kubwa za kudhibiti ujangili.
Aidha, Katika mfumo ikolojia wa Serengeti idadi ya nyumbu imeongezeka kutoka1,326,709 mwaka 2015 hadi 1,597,850 mwaka 2022 na katika mfumo ikolojia wa Nyerere-Selous-Mikumi matokeo ya sensa yanaonesha mfumo huo una nyumbu 19,000.
Pia. Matokeo ya sensa Katika mfumo ikolojia wa Nyerere-Selous-Mikumi yanaonesha idadi ya tembo imeongezeka kutoka 15,501 mwaka 2018 hadi 20,006 mwaka 2022 na ujangili wa tembo umepungua kutoa asilimia16% mwaka 2018 hadi 0.8% mwaka 2022.
Ikumbukwe takwimu hizi ni za mifumo mitatu (3) ya ikolojia kati ya mifumo kumi na moja (11) nchini, hivyo🇹🇿 tunaujasiri wa kujivunia utajiri huu wa malisili ya wanyamapori