MRADI WA UTAFITI WA SIMBA CHACHU YA UTALII SERENGETI

Taarifa za kisayansi zinazotokana na Mradi wa muda mrefu wa Utafiti wa SIMBA SERENGETI unaoratibiwa na Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) kupitia Kituo cha Utafiti wa Wanyamapori Serengeti, zimekua chachu katika uhifadhi na kivutio cha Utalii ndani ya hifadhi ya Taifa Serengeti.

Mradi huu wa SIMBA SERENGETI unafuatilia idadi, tabia na mienendo ya makundi ya simba kwa zaidi ya miaka 50, ambapo kwa sasa yapo makundi 20 yenye jumla ya simba takribani 300 yanayofuatiliwa.

Aidha, Katika mradi wa SIMBA SERENGETI utambulisho hufanyika kwa kila Simba kuandaliwa kadi maalumu (Lion identification card) kwa kutumia alama/madoa ya Kipekee kwenye uso eneo la ndevu (Whisker spots) na alama nyinginezo za asili.Utambulisho huu husaidia kumfuatilia simba mmoja mmoja ndani ya kundi.

Aidha matumizi ya teknolojia yanarahisisha utafiti wa simba ambapo kwa kutumia mikanda ya simba yenye redio za mawasiliano (VHF/GPS satellite collars) anayofungwa simba jike katika kila kundi unasaidia kujua kundi lipo wapi.

Taarifa za kisayansi za utafiti zinatoa dira katika kuwahifadhi Simba, kunadi Utalii kupitia takwimu na tabia za simba, ikikumbukwa Simba ni Miongoni mwa Wanyamapori wakubwa ambao ni kivutio cha utalii (major tourism attraction) ambaye watalii wengi wanapenda kumuona wanapokuja kwenye hifadhi.

Tafiti za wanyamapori kwa ustawi wa uhifadhi na kukuza utalii nchini🇹🇿

Visitors

033853
Users Today : 19
Users Last 7 days : 624
Users This Month : 1565
Total Users : 33853

Office Location

Contact Us