SERENGETI CHIMBUKO LA UTAFITI WA WANYAMAPORI TANZANIA

Kituo cha Utafiti wa Wanyamapori Serengeti (SWRC) ni miongoni mwa vituo vitano vya Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) kinachobeba historia ya chimbuko la tafiti za wanyamapori hapa nchini ambapo tafiti zilianza miaka ya 1950.

Kituo hiki ndipo historia ya TAWIRI ilpoanzia kwani awali, kwa mujibu wa Sheria ya Bunge Na.4 ya mwaka 1980 kilianzishwa kama Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Serengeti (SRI) na mwaka 1999, kwa mujibu wa Sheria ya Bunge Na.10 (CAP 260 REF 2002), Taasisi hiyo ikabadilishwa Jina la kuwa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) ikiwa na jukumu kuu la kufanya, kuratibu na kusimamia tafiti za wanyamapori hapa nchini🇹🇿

Serengeti Shall never die

Visitors

027082
Users Today : 0
Users Last 7 days : 450
Users This Month : 1008
Total Users : 27082

Office Location

Contact Us