SERIKALI YAENDELEZA JITIHADA ZA KUREJESHA MBWA MWITU HIFADHI YA TAIFA SERENGETI

Serikali kupitia Taasisi zake TAWIRI na TANAPA imeendelea na zoezi endelevu la kuwarejesha mbwa mwitu ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ikiwa ni kuhakikisha mbwa mwitu wanaendelea kuhifadhiwa katika mfumo ikolojia ya Serengeti.

Akizungumza wakati wa zoezi la kuwapokea mbwa mwitu wapatao 20 waliozaliwa Hifadhi ya Taifa Mkomazi na kuletwa Hifadhi ya Taifa Serengeti kabla ya kuachiwa huru, Dkt. Emmanuel Masenga ambaye ni Mtafiti Mkuu na Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti Serengeti amesema kuwa matokeo ya tafiti yanaonyesha kuwa sababu kuu za kutoweka kwa mbwa mwitu katika hifadhi ya Serengeti ni magonjwa (Rabies and Canine Distemper Virus) na ongezeko la idadi ya simba na fisi pamoja na kuuwawa na wananchi wanapotoka nje ya hifadhi.

Aidha, Dkt. Masenga amesema jitihada za Serikali za kuwarejesha mbwa mwitu ndani ya Hifadhi ya Taifa Serengeti ni zoezi endelevu na lilianza tangu mwaka 2011 kwa lengo la kuhifadhi mbwa mwitu kwa ajili ya kutunza bioanuwai na kuendeleza utalii.

Dkt. Masenga amesema kama inavyofahamika jukumu kubwa la Taasisi ya Utafiti Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) ni kufanya tafiti za wanyamapori, hivyo TAWIRI inaendelea kufanya tafiti za kina za kuhakikisha kuwa mbwa mwitu wanaendelea kuhifadhiwa katika mfumo ikolojia wa Serengeti.

Visitors

031670
Users Today : 1
Users Last 7 days : 393
Users This Month : 1186
Total Users : 31670

Office Location

Contact Us