TANZANIA YAONGOZA KWA IDADI KUBWA YA SIMBA, CHUI NA NYATI BARANI AFRIKA

Tanzania inaendelea kujivunia kuwa na utajiri mkubwa wa Rasilimali ya Wanyamapori ambapo inashikilia nafasi ya kwanza barani Afrika kwa kuwa na idadi kubwa ya Simba, Chui na Nyati.

Haya yalibainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) Dkt. Eblate Ernest Mjingo katika hafla ya uzinduzi wa matokeo ya sensa ya wanyamapori katika mifumo ikolojia mitatu ya Nyerere-Selous-Mikumi, Saadani-Wamimbiki na Serengeti.

Dkt. Mjingo alieleza kuwa, kwa mujibu wa taarifa ya Umoja wa Kimataifa wa Uhifadhi na Kulinda Uasilia (IUCN) ya mwaka 2023, Tanzania inaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya simba barani Afrika, ambapo ina jumla ya simba elfu 17, ikifuatiwa na Afrika Kusini yenye simba 3,300 na Botswana yenye Simba 3,064.

Vilevile, kwa upande wa nyati Tanzania inashika nafasi ya kwanza kwa kuwa na nyati 225,000, ikifuatiwa na Afrika Kusini yenye nyati elfu 46 na ya tatu ni Msumbiji yenye nyati elfu 45.

Kwa upande wa chui Tanzania inaendelea kushika rekodi ya kwanza kwa kuwa na idadi ya chui elfu 24 sambamba na kushika nafasi ya tatu kwa kuwa na tembo elfu 60.

Aidha, Dkt. Mjingo amebainisha hali ya ustawi wa uhifadhi wa wanyamapori hapa nchini ni kutokana na juhudi kubwa za Serikali katika kuhifadhi ambapo imeendelea kuwezesha tafiti mbalimbali kufanyika pamoja na sensa za wanyamapori sambamba na mchango mkubwa wa usimamizi na ulinzi shirikishi wa Mamlaka za Uhifadhi za TANAPA, TAWA na Ngorongoro .

Visitors

033906
Users Today : 72
Users Last 7 days : 677
Users This Month : 1618
Total Users : 33906

Office Location

Contact Us