TAWIRI YATOA MAFUNZO WILAYA TANO ZENYE MGONGANO KATI YA BINADAMU NA TEMBO

Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) inatekeleza jitihada za Wizara ya Maliasili na Utalii za kutatua changamoto ya Binadamu na Wanyamapori hususani tembo kwa kutoa mafunzo ya mbinu za kuepuka madhara na uharibifu wa tembo kwa wananchi.

Mafunzo hayo ya nadharia na vitendo yametolewa kwa wananchi, Askari wa Wanyamapori wa Vijiji (VGS) na askari Wa TAWA kutoka wilaya za Nkasi, Mbarali ,Iringa, Manyoni Itigi ambazo ni miongoni mwa Wilaya 91 zinazokabiliwa na changamoto hiyo nchini.

Aidha, wananchi wamejifunza tabia za tembo ili kuepuka madhara , mbinu za kuzuia uharibifu wa tembo mashambani kwa kutumua fensi ya mizinga ya nyuki, fensi za vitambaa vya pilipili na oili chafu, matofali ya pilipili , kilimo cha mazao mbadala ( pilipili, Alizeti ya katamu , Tangawizi .

vilevile mbinu za kumuondoa tembo kwenye makazi ya watu kwa kutumia tochi zenye mwanga mkali, Vuvuzela maalum, vifaa vyenye mlipuko ambavyo hutumika kwa utaratibu maalum.

TAWIRI KISIMA CHA SAYANSI YA WANYAMAPORI

Visitors

037076
Users Today : 7
Users Last 7 days : 513
Users This Month : 513
Total Users : 37076

Office Location

Contact Us