USAMBAZAJI MATOKEO YA TAFITI ZA WANYAMAPORI

Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) ikiwa ni taasisi ya kimkakati katika sekta ya uhifadhi na Utalii , yenye jukumu la Kufanya, Kuratibu na Kusimamia Tafiti za Wanyamapori hapa nchini imeendelea kutumia majukwaa mbalimbali kusambaza matokeo ya tafiti za wanyamapori na elimu ya sayansi kwa ujumla ili kuimarisha uhifadhi na kukuza utalii nchini.

Leo Tarehe 11 Desemba 2024 watafiti wa TAWIRI ni miongoni mwa washiriki wa Kongamano la tatu la Kisayansi la Kimataifa la Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI) linalofanyika kwa siku tatu kuanzia leo hadi tarehe 13 Desemba,2024 katika ukumbi wa AICC Jiji la Arusha.

Mgeni rasmi wa Kongamano hilo ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayewakilishwa na Naibu Waziri,Wizara ya Maliasili na Utalii Mhe. Dunstan Kitandula.

TAWIRI kisima cha sayansi ya wanyamapori nchini

Visitors

033783
Users Today : 119
Users Last 7 days : 647
Users This Month : 1495
Total Users : 33783

Office Location

Contact Us