WAZIRI KAIRUKI AIPONGEZA TAWIRI KWA ZAO JIPYA LA UTALII WA KITAFITI

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) ameipongeza Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) kwa zao jipya la utalii wa kitafiti na kuitaka kuendelea kufanya tafiti za kitalii na kutoa mapendekezo ya mazao mapya ya utalii ili kuendelea kukuza sekta ya uhifadhi na utalii chini.

Mhe. Kairuki amesema hayo alipofanya ziara kwenye taasisi hiyo na kuzungumza Menejimenti na watumishi wa TAWIRI katika makao makuu ya taasisi hiyo Njiro – Arusha, ambapo ameitaka TAWIRI kujitangaza ndani na nje ya nchi na kutoa ushauri wa kitaalamu kwa taasisi nyingine.

” Muendelee kuzitangaza tafiti zenu kimataifa ili zitumike katika mataifa mengine ” amehimiza Mhe. Kairuki .

Mkurugenzi Mkuu TAWIRI Dkt.Eblate Ernest Mjingo amesema TAWIRI imepokea maelekezo ya Mhe.Waziri ambapo pia amemshukuru kwa ziara na kufafanua TAWIRI imeendelea kufanya tafiti za wanyamapori na kutoa ushauri wa kitaalamu ili kuimarisha sekta ya uhifadhi na kukuza utalii nchini.

Visitors

031670
Users Today : 1
Users Last 7 days : 393
Users This Month : 1186
Total Users : 31670

Office Location

Contact Us