WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII AFANYA ZIARA YA KIKAZI TAWIRI

Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana(Mb) amefanya ziara katika makao makuu ya Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) Njiro – Arusha, ambapo amebainisha umuhimu wa Tafiti za Wanyamapori katika kupata takwimu za Kisayansi zinazotumika kufanya maamuzi.

Akizungumza katika kikao na Menejimenti ya TAWIRI Mhe. Chana amesema Serikali inatumia takwimu za kisayansi kufanya maamuzi yaliyojikita kuimarisha uhifadhi wa Wanyamapori ili kuwa na Utalii endelevu.

” Tunahakikisha rasilimali hii ya Wanyamapori ipo kwa kizazi cha leo na kijacho ambapo matumizi ya takwimu za kisayansi ni dira katika uhifadhi amesisitiza Waziri Chana.

Mkurugenzi Mkuu TAWIRI Dkt.Eblate Mjingo amesema takwimu za tafiti zinasaidia kunadi Utalii ikiwa ni pamoja na kuelekeza namna bora ya kufanya Utalii sambamba na kuimarisha uhifadhi.

Aidha, Pamoja na mambo mengine Waziri Chana amepokea taarifa mbalimbali za utendaji kazi wa Taasisi hiyo.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Utalii, Nkoba Mabula, Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Dkt. Thereza Mugobi, wawakilishi kutoka Idara ya Wanyamapori Wizara ya Maliasili na Utalii na Maafisa Waandamizi kutoka TAWIRI.

Visitors

031670
Users Today : 1
Users Last 7 days : 393
Users This Month : 1186
Total Users : 31670

Office Location

Contact Us